Competition in this pair is now closed, and the winning entry has been announced. Discussion and feedback about the competition in this language pair may now be provided by visiting the "Discussion & feedback" page for this pair. Entries may also be individually discussed by clicking the "Discuss" link next to any listed entry. Source text in English The moment when, 50 years ago, Neil Armstrong planted his foot on the surface of the Moon inspired awe, pride and wonder around the world. This newspaper argued that “man, from this day on, can go wheresoever in the universe his mind wills and his ingenuity contrives…to the planets, sooner rather than later, man is now certain to go.” But no. The Moon landing was an aberration, a goal achieved not as an end in itself but as a means of signalling America’s extraordinary capabilities. That point, once made, required no remaking. Only 571 people have been into orbit; and since 1972 no one has ventured much farther into space than Des Moines is from Chicago.
The next 50 years will look very different. Falling costs, new technologies, Chinese and Indian ambitions, and a new generation of entrepreneurs promise a bold era of space development. It will almost certainly involve tourism for the rich and better communications networks for all; in the long run it might involve mineral exploitation and even mass transportation. Space will become ever more like an extension of Earth—an arena for firms and private individuals, not just governments. But for this promise to be fulfilled the world needs to create a system of laws to govern the heavens—both in peacetime and, should it come to that, in war.
The development of space thus far has been focused on facilitating activity down below—mainly satellite communications for broadcasting and navigation. Now two things are changing. First, geopolitics is stoking a new push to send humans beyond the shallows of low-Earth orbit. China plans to land people on the Moon by 2035. President Donald Trump’s administration wants Americans to be back there by 2024. Falling costs make this showing off more affordable than before. Apollo cost hundreds of billions of dollars (in today’s money). Now tens of billions are the ticket price.
[ … ]
It is a mistake to promote space as a romanticised Wild West, an anarchic frontier where humanity can throw off its fetters and rediscover its destiny. For space to fulfil its promise governance is required. At a time when the world cannot agree on rules for the terrestrial trade of steel bars and soybeans that may seem like a big ask. But without it the potential of all that lies beyond Earth will at best wait another 50 years to be fulfilled. At worst space could add to Earth’s problems. | The winning entry has been announced in this pair.There were 4 entries submitted in this pair during the submission phase. The winning entry was determined based on finals round voting by peers.
Competition in this pair is now closed. | Miaka 50 iliyopita, wakati ambapo Neil Armstrong alitua kwenye Mwezi, aliibua hofu, fahari na kuwaduwaza watu kote duniani. Gazeti hili lilidai kwamba "kuanzia siku ya leo, binadamu anaweza kuenda popote ulimwenguni ambapo akili yake inataka na apange kupafikia... kwenye sayari mbalimbali, hivi karibuni, binadamu sasa ana uhakika wa kuenda." Ila, kutua kwenye Mwezi kulikuwa sio shabaha hasa, ni lengo lililofikiwa sio kama mpango kamili lakini kama namna ya kuashiria uwezo usio wa kawaida wa Marekani. Hoja hiyo, pindi tu ilipowekwa, haikuhitaji kuwekwa tena. Ni watu 571 pekee ambao wamewahi kufika kwenye uzingo; na tangu 1972 hakuna mtu mwingine ambaye amefikia anga kuliko alivyofanya Des Moines kutoka Chigaco. Miaka 50 ijayo itakuwa tofauti sana. Gharama kushuka, kuwepo kwa teknolojia mpya, azma ya Uchina na India pamoja na kizazi kipya cha wajasiriamali kunaahidi enzi dhabiti ya maendeleo ya anga. Itahusisha pakubwa utalii kwa ajili ya mitandao mahiri na bora ya mawasiliano kwa watu wote; hatimaye huenda ikahusisha shughuli ya uchimbaji wa madini na hata usafirishaji kwa kiasi kikubwa. Anga itakuwa kama sehemu ya Dunia—jukwaa la mashirika na watu binafsi, sio tu serikali mbalimbali. Lakini, ili ahadi hii itimizwe, ulimwengu unahitaji kuweka mfumo wa sheria ili kuongoza mbingu—wakati wa amani na pia wakati wa vita, endapo ulimwengu utajipata hapo. Maendeleo ya anga hivyo yamekuwa yakiangazia shughuli ya kupiga jeki shughuli zilizo hapa chini - hususan mawasiliano ya setilaiti kwa ajili ya upeperushaji wa matangazo na usogezaji. Sasa mambo mawili yanabadilika. Kwanza, siasa za ulimwenguni zinaibua msukumo mpya kwa binadamu zaidi ya kufikia tu eneo la juujuu la uzingo wa Dunia. Uchina ina mpango wa kutua watu kwenye Mwezi kufikia 2035. Utawala wa Rais Donald Trump unataka Wamarekani kurejea pale kufikia 2024. Kushuka kwa gharama kunafanya majigambo haya kuwa ya bei nafuu zaidi kuliko hapo awali. Mradi wa Apollo uligharimu mabilioni ya dola (katika pesa ya leo). Sasa, mabilioni kadhaa ndiyo bei ya tiketi. [… ] Ni kosa kutangaza anga kama inavyofanywa filamu ya mahaba ya Wild West, ambayo ni filamu ya mgogoro ambapo binadamu wanaweza kutupilia mbali pingu zinazowafunga na kugundua mustakabali wao upya. Ili anga itimize ahadi yake, utawala unahitajika. Wakati ambapo ulimwengu hauwezi kukubaliana kuhusu kanuni za biashara ya vyuma na mbegu ya soya, hii huenda ikawa hoja kubwa. Lakini bila kufanya hivyo, uwezo wa yote yaliyopo mbali na Dunia utasubiri kwa muda mwingine wa angalau miaka 50 ili utimizwe. Anga ina uwezekano mdogo wa kuongeza matatizo ya Dunia. | Entry #27230 — Discuss 0 — Variant: Kenyankenyswa
Winner Voting points | 1st | 2nd | 3rd |
---|
54 | 12 x4 | 3 x2 | 0 |
- 3 users entered 5 "like" tags
alitua kwenye Mwez | Good term selection | Grace Njenga No agrees/disagrees | |
alitua kwenye Mwezi, | Flows well | Grace Njenga No agrees/disagrees | |
Anga itakuwa kama sehemu ya Dunia | Good term selection | Kevin Juma No agrees/disagrees | |
Utawala wa Rais Donald Trump unataka Wamarekani kurejea pale kufikia 2024. | Flows well | Kevin Juma No agrees/disagrees | |
Anga ina uwezekano mdogo wa kuongeza matatizo ya Dunia. | Flows well It conveys the intended meaning upon the context. | Carolyne Mumo Musyoka No agrees/disagrees | |
| Miaka 50 iliyopita, wakati ambapo Neil Armstrong alipowacha alama ya kanyago lake huko mwezini, tukio hilo liliwatia hofu, kuwapa fahari na likawa kama muujiza mkubwa ulimwenguni kote. Gazeti hili lilidadisi kwamba “kutoka leo, mtu anaweza kutembea mahali popote anapotaka duniani iwapo tu fikra zake zinamtuma kufanya hivyo pamoja na ubunifu wake wa kimaarifa…katika sayari, tena haraka iwezekanavyo,mtu sasa ameamua kutembea.” Lakini hapana. Kitendo cha kufika mwezini hakikuwa cha kawaida, lengo lililofikiwa halikuwa ndio matarajio yenyewe bali lilikuwa kama nyenzo tu ya kuudhihirishia ulimwengu kuhusu uwezo wa kipekee wa Marekani. Pindi tu hoja hiyo ilipotolewa, haikuhitaji kuundwa upya. Ilikuwa ni watu 571 pekee ambao walikuwa wamewahi kutembelea sayari; na kutokea 1972 hapakuwa na mtu aliyekuwa ameenda mbali katika anga za juu kuliko Des Moines kutoka Chicago. Miaka 50 ijayo itakuwa tofauti sana. Kushuka kwa bei, teknolojia mpya, maazimio ya wachina na Wahindi, pamoja na kizazi kipya cha wajasiriamali kinachoahidi kipindi cha mabadiliko ya anga. Bila shaka itahusisha utalii kwa matajiri na mitandao ya mawasiliano bora kwa watu wote; baada ya muda inaweza kuhusisha uchimbaji wa madini na uchukuzi wa watu wengi. Anga itakuwa kama sehemu ya Ardhi – ukumbi wa mashirika na watu binafsi, sio tu Serikali. Lakini ili kutimizwa kwa ahadi hii, ulimwengu unahitaji kuunda mifumo ya kisheria ili kusimamia anga – katika muda wa kawaida na, itakapotokea, katika vita. Kwa hivyo, maendeleo ya angani yamezingatia kushughulikia matukio yaliyo ardhini – hususan mawasiliano ya wambiyo kwa ajili ya kutangaza pamoja na urambazaji. Hivyo basi, mambo mawili yanabadilika hapa. Kwanza, siasa za kikanda zinachukua matao ya juu na kuwasababishia wanadamu madhila kwenye mzunguko wa ardhi. Uchina ina mipango ya kuwapeleka watu mwezini kufikia 2035. Mamlaka ya usimamizi wa Rais Donald Trump wanawataka Wamarekani kurudi mwezini kufikia 2024. Kushuka kwa bei kunasababisha kuwepo kwa mbwembwe hizi na kuifanya gharama kuwa nafuu zaidi ukilinganisha na hapo awali. Apollo iligharimu mamia ya mabilioni ya madola (katika pesa za sasa). Hivi sasa, makumi ya mabilioni ni gharama ya tikiti. […] Ni kosa kupigia debe shughuli za angani kama zinavyopendwa kwenye Mbuga za Magharibi, eneo la kale ambapo walimwengu wanaweza kutupilia mbali mambo yao na kuvumbua hatima yake. Ili anga itimize ahadi yake, panahitajika usimamizi bora. Katika nyakati ambazo dunia haiwezi kukubaliana kuhusu masharti ya biashara ya chuma ya kimaeneo pamoja na maharage ya Soya yanayoweza kuonekana kama ombi kubwa. Lakini vinginevyo, uwezekano wa vitu vyote vilivyoko nje ya ardhi vitalazimika kungojea miaka mingine 50 ili kutimizwa. Baya zaidi ni kuwa anga inaweza kuzidisha matatizo ya Ardhi. | Entry #27751 — Discuss 0 — Variant: Kenyankenyswa
Voting points | 1st | 2nd | 3rd |
---|
44 | 10 x4 | 2 x2 | 0 |
- 7 users entered 7 "like" tags
- 4 users agreed with "likes" (7 total agrees)
- 1 user disagreed with "likes" (1 total disagree)
Miaka 50 iliyopita, wakati ambapo Neil Armstrong alipowacha alama ya kanyago lake huko mwezini, tukio hilo liliwatia hofu, kuwapa fahari na likawa kama muujiza mkubwa ulimwenguni kote. | Flows well Very natural rendition, reading as though it was originally written in Swahili | Matthias Kavuttih No agrees/disagrees | |
-1 +4 4 kanyago | Good term selection excellent choice of word | Joan Njogu | |
+2 2 Pindi tu hoja hiyo ilipotolewa | Flows well Good start of the sentence | Peter Wachira | |
Miaka 50 ijayo itakuwa tofauti sana | Flows well Nimeipenda hii. | Kibwe Amani Yao No agrees/disagrees | |
hususan mawasiliano ya wambiyo kwa ajili | Flows well | Faith Mueni No agrees/disagrees | |
makumi ya mabilioni ni gharama ya tikiti | Flows well | Kevin Juma No agrees/disagrees | |
| Wakati ambapo, takriban miaka hamsini iliyopita, Neil Armstrong aliweza kupaa hadi anga za mwezi ni wakati uliowaduwaza wengi, ukawapa wengi kujivunia na hata mshangao ulimwenguni kote. Kwenye jarida hili, ilitabiriwa kwamba, toka siku hii, binadamu ana uwezo wa kwenda popote pale ulimwengu mzima fikra zake zitamruhusu na pia ufahamu wake ufikapo...kwa sayari zote, na kwa hakika binadamu yupo tayari kwenda. Lakini sivyo. Kufika kwa mwezi kuliashiria muamko mpya, sio tu kuonyesha uwezo wa kufika mahali pale bali pia kama jinsi ya Marekani kuonyesha ukakamavu wake duniani.. Kwa kweli marekani ilifaulu kudhihirisha ukakamvu wake. Ni watu mia tano sabini na moja pekee ndio wameweza kupaa hadi kwa mwezi kwa kipindi hiki; Na tangu mwaka wa 1972, hakuna aliyeweza kuenda zaidi ya Armstrong kwa umbali uliozidi des Moines ilipo na Chicago. Miaka hamsini ijayo itakuwa todfauti sana. Gharama za chini, teknolojia mpya, matamanio ya uchina na India na pia kizazi kipya cha wajasiriamali; Yote haya yataashiria mwamko mpya kuendeleza juhudi za safari za anga. Pasi na kujumuisha utalii kwa matajiri na kuimarisha mitandao ya mawasiliano kwa wote; mwishowe kuna uwezekano wa kutumia safari hizi kuchimba madini na hata usafiri wa uma. Anga zitakuwa tu kama sehemu ya ardhi-uwanja wa mashirika na pia watu binafsi, na sio tu ya serikali. Na, kwa haya yote kutimizwa, kuna umuhimu wa kuunda mfumo wa sheria zitakazo ongoza maswala ya safari za anga, wakati wa amani na wakati wa vita kama ipasavyo. Teknolojia ya safari za anga hadi sasa imeangazia shughuli za hapa hapa duniani haswa mawasiliano ya satelaiti kwa minajili ya utangazaji na pia urambazaji. Cha msingi, mambo mawili yanabadilika. Kwanza, siasa, haswa mahusiano ya kimataifa zinaleta msukumo kwa mataifa kwa minajili ya kutaka kutuma binadamu zaidi ya safari za ndege. Uchina inapania kutua watu kwenye mwezi ifikapo mwaka wa 2035. Serikali ya marekani chini yake Rais Donald Trump inatarajia kutua ifikapo mwaka wa 2024. Kadri gharama zinavyopunguka ndivyo shughuli hii inavyozidi kuwa nafuu ikilinganishwa na hapo awali. Safari ya kwanza ya Apollo iligharimu mamia ya bilioni dola (pesa za leo). Kwa sasa, tiketi ya mtu mmoja inagharimu chini ya bilioni mia moja. Ni kosa kukabili suala hili bila kuzingatia maadili na sheria, Utaratibu wa kisheria unatakikana kama mojawazo ya kanuni za kuwezesha safari za anga. Hata hivyo, Itakuwa ni vigumu sana kufanya hivi tukizingatia kwamba mataifa yameshindwa kuzingatia sheria zilizoko katika uuzaji wa vitu vigdogo vidogo kama chuma na hata soya. Ilhali, bila technolojia hii, yote binadamu alikusudia katika safari za anga itangoja miaka zingine hamsini kutimizwa. Anga huenda ikawa hata chanzo cha shida zaidi duniani. | Entry #27551 — Discuss 0 — Variant: Not specifiednone
Voting points | 1st | 2nd | 3rd |
---|
8 | 1 x4 | 1 x2 | 2 x1 |
- 3 users entered 3 "dislike" tags
- 1 user agreed with "dislikes" (1 total agree)
aliweza kupaa hadi anga za mwez | Inconsistencies | Grace Njenga No agrees/disagrees | |
| Wakati ambapo, miaka 50 iliyopita, Neil Armstrong alipanda mguu wake juu ya uso wa Mwezi aliongoza mshtuko, kiburi na mshangao kote ulimwenguni. Gazeti hili lilisema kwamba "mwanadamu, tangu siku hii kuendelea, anaweza kwenda popote kwa akili ya ulimwengu na mapenzi yake yanafanya mambo mazuri ... kwa sayari, mapema badala ya baadaye, mwanadamu sasa atatakiwa kwenda." Lakini hapana. Kutua kwa Mwezi ilikuwa uhamishaji, lengo halikufanikiwa yenyewe kama mwisho lakini kama njia ya kuashiria uwezo wa ajabu wa Amerika. Uhakika huo, ukiwa umetengenezwa, haukuhitaji kurejea tena. Ni watu 571 tu ambao wameingia kwenye mzunguko na tangu 1972 hakuna mtu aliyeingia mbali zaidi katika nafasi kuliko Des Moines ni kutoka Chicago. Miaka 50 ijayo itaonekana tofauti sana. Gharama za kuporomoka, teknolojia mpya, matamanio ya China na India, na kizazi kipya cha wajasiriamali huahidi enzi ya ujasiri wa maendeleo ya nafasi. Karibu itahusisha utalii kwa mitandao tajiri na bora ya mawasiliano kwa wote; mwishowe inaweza kuhusisha unyonyaji wa madini na hata usafirishaji mkubwa. Nafasi zitakuwa kama nafasi ya kupanuliwa kwa Dunia - uwanja wa makampuni na watu binafsi, sio serikali tu. Lakini ili ahadi hii ikamilike ulimwengu unahitaji kuunda mfumo wa sheria kutawala mbingu- kwa wakati wa amani na, ikiwa itafika kwa vita. Uboreshaji wa nafasi hadi sasa umezingatiwa katika kuwezesha shughuli chini chini - mawasiliano ya setileti kwa utangazaji na urambazaji. Sasa mambo mawili yanabadilika. Kwanza, jiografia inasukuma kushinikiza mpya kutuma wanadamu zaidi ya shina la mzunguko wa chini wa Dunia. Uchina unapanga kutua watu juu ya Mwezi ifikapo mwaka 2035. Utawala wa Rais Donald Trump unataka Wamarekani warudi huko ifikapo 2024. Gharama za kushuka hufanya hii kuonyesha kuwa ya bei nafuu zaidi kuliko hapo awali. Apollo aligharimu mamia ya mabilioni ya dola (katika pesa za leo). Sasa makumi ya mabilioni ni bei ya tikiti. […] Ni kosa kukuza nafasi kama pori la pori la kimapenzi, ukingo wa anarchic ambapo ubinadamu unaweza kutupa turubaa zake na kugundua umilele wake. Kwa nafasi ya kutekeleza ahadi yake ya utawala inahitajika. Kwa wakati ambao ulimwengu hautakubaliana juu ya sheria za biashara ya ulimwengu ya baa za chuma na soya ambazo zinaweza kuonekana kama swali kubwa. Lakini bila hiyo uwezo wa yote yaliyo juu ya Dunia yatasubiri miaka 50 zaidi kutimizwa. Katika nafasi mbaya zaidi inaweza kuongeza shida za Dunia. | Entry #27565 — Discuss 0 — Variant: Kenyankenyswa
Voting points | 1st | 2nd | 3rd |
---|
0 | 0 | 0 | 0 |
- 1 user entered 1 "dislike" tag
Wakati ambapo, miaka 50 iliyopita, Neil Armstrong alipanda mguu wake juu ya uso wa Mwezi aliongoza mshtuko | Syntax The syntax is not native to Swahili | Matthias Kavuttih No agrees/disagrees | |
| | | | | X Sign in to your ProZ.com account... | | | | | | ProZ.com translation contestsProZ.com translation contests offer a fun way to take a break from your normal routine while testing and honing your skills with fellow translators.
ProZ.com Translation Contests. Patent pending. |