Mwanzo wake
Miaka mingi iliyopita, mambo mengi yaliyotokea kwa wakati mmoja,
Ujana ukapita na hatimaye nikawa mtu mzima:
Kwa ghafta tu, maisha yangu yakaanza!
Niliuona ulimwengu mbele yangu— Kwa hivyo,
Mkulima yule akawa amesimama na farasi wake
Huku akitokwa na jasho jembamba kwenye upaji wake wa uso,
Baada ya kuondoka kwenye maeneo ya vitivo vya mto
Nikalima mitaro kwenye mharara ulio upande wa chini,
Na kuona upande mmoja wa mlima kwa ajili ya kilimo,
Jangwa lenye mwamba butu na lisiloweza kupandwa kitu,
Ngurumo na radi zikitamalaki angani,
Na wingu jeusi kwenye kilele, likaangama,
Sasa nasubiria tu.
—Muwache alime sehemu hiyo iwapo atathubutu!